Sura ya Kwanza
Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu
------------------------------------------
Sura ya Pili
Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.
---------------------------------
Sura ya Tatu
Je! Yesu ni nani haswa?
---------------------------------
Sura ya Nne
Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?
---------------------------------
Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com
WASIFU WA YESU KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA
Je Yesu Alimtabiri Mtume Muhammad kKatika Yohana 16:7
Mapitio ya mada
-
Nini maana,aina na kazi za Roho?.
-
Je Roho wa kweli anayetabiriwa na Yesu Yoh 16:7 ni Muhammad?
-
Maelezo ya Qur an juu ya Roho.
-
Maana ya Roho
Tasfiri ya neno Roho katika msingi wa imani ya kikristo inatolewa kwa kurejea katika vyanzo vya lugha za asili za kibiblia kama ifuatavyo:-
Kiebrania “{Ebrew}” ni – Rua’ch ……
Kiyunani “ {Greec }” ni – Pne’uma ….
Lugha hizo zote zinazohusika kutaja roho humaanisha“Pumzi na si vinginevyo.
Katika sehemu nyingine ya maandiko ya Biblia Bwana Yesu anaweka wazi kuwa roho katika aina zake ni kitu kisicho na mifupa.
Luka 24:36-39 Roho haina mifupa…………
2. Aina za Roho
Katika maandiko ya Biblia tunaweza kuona kuwepo kwa aina tatu za Roho katika vifungu mbalimbali vya maandiko yake kama inavyoonekana:-
- Roho ya uhai
Mwanzo 2:7 akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.
Qur an 15:29 Basi nitakapo makamilisha na kumpulizia roho inayotokana
na mimi basi mmuangukie na kumtii.
Hivyo hapo tunajifunza kuwepo kwa roho ya uhai
- Roho mtakatifu
Luka 4:17 roho wa Bwana yu juu yangu……..
Luka 1:35 roho mtakatifu / nguvu
Qur an 5:110 kumbukeni tena Mwenyezi Mungu atakapo sema, ewe Isa mwana
wa Mariam kumbuka neema yangu juu yako, nilipo kusaidia kwa
kukupa kuwa na wewe roho takatifu.
Hapo Biblia hueleza kuwepo kwa roho mtakatifu ambaye kwa kadri ya Biblia
alikuwa na jukumu katika kuwawezesha wajumbe wa Mungu Kunena maneno ya
Mungu kwa ufunuo na ujasiri wote.
- Roho za mashetani
1Timotheo 4:1-2 roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu
watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo na
mafundisho ya mashetani.
Waefeso 2:1 roho atendaye kazi katika wana wa kuasi.
Nina imani kuwa ndugu msomaji wangu tunakwenda sambamba katika mada hii nzuri, hivyo Biblia imetuwezesha kutambua kuwepo kwa aina hizo tatu za roho. Lakini katika mada hii aina ya roho inayoonekana kutuingiza kwenye mjadala huu ni ya pili yaani roho mtakatifu ambaye kimsingi ndiye aliyekuwa akitabiriwa na Bwana Yesu katika kitabu cha Yohana 16:7 na hivyo baadhi ya mafundisho ya dini humnasibisha na mtume Muhammad.
3. Je roho wa kweli anayetabiriwa na Yesu Yohana 16:7 ni Muhammad?
Ni kwa miaka mingi sasa fundisho la kudai kuwa Biblia inamtabiri Muhammad kupitia ahadi ya Yesu ya kuleta msaidizi limekuwa likitolewa na wahadhiri mabalimbali wa kiislam kupitia mikutano yao ya hadhara,kanda za audio na video pamoja na njia ile ya uandishi wa vitabu.
Ili kuelewa ukweli wa changamoto hii, hatua ya makusudi ya kuchunguza vitabu inapaswa kuchukuliwa, hatua hii ya kiuchunguzi ili iweze kuzaa matunda inapaswa ihusike na kuangalia sifa na tabia mbalimbali za kimsingi zinazo mhusu huyo anayenenwa katika utabiri huo wa Yesu na kuzilinganisha na Muhammad ili kuona, endapo kuna ulinganifu wowote wa kweli unaoweza kutoa picha ya kuhusika kwa Muhammad katika utabiri huo wa msaidizi wa Yesu.
Mhubiri 7:27 tazama asema mhubiri mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha
hili na lile ili kupata jumla ya mambo hayo...
Sifa za roho / Msaidizi Muhammad
1 Yohana 14:16 akae nanyi hata milele Qur an 39:30 kwa yakini wewe
utakufa,na wao pia watakufa.
2 Yohana 14:17 roho wa kweli ambaye Qur an 74:1-3 ewe uliyejifunika maguo
ulimwengu hauwezi kumpokea simama uonye viumbe na Mola wako
kwakuwa haumwoni. umtukuze na nguo zako uzisafishe.
3. Yohana 16:8 atauhakikisha ulimwengu Fuatilia uchambuzi nje ya chati
kwa habari ya haki, dhambi na hukumu
Katika maelezo ya aya hiyo ya Yohana 16:8 Biblia inataja aki mahususi ambazo huyo msaidizi atakuja kuzifanya, nazo ni Kuuhakikishia ulimwengu juu ya habari ya mambo makuu matatu ya msingi nayo ni;
-
Dhambi
-
Haki
-
Hukumu
Sehemu hii ya maelezo ya Biblia pamoja na mambo mengine lakini imezua utata na hoja nyingine kwa wale wanaotamani ubashiri huu uangukie kwa Muhammad, fatilia hoja nyingine inayoibuliwa hapa pamoja na majibu yake kwa jumla.
Hoja inayoibuka
Maelezo ya Biblia yanaonyesha kuwa huyo roho anapo kuja atafanya kazi ya kuuhakikishia ulimwengu kwa habari ya mambo mbalimbali kama yalivyo orodheshwa katika aya hiyo.
Swali;
Ikiwa roho huyo si mwanadanu bali roho mtakatifu je”roho mtakatifu ana mdomo wa kunena?
Jibu;
Ili kulielewa hilo kwa uzuri nivyema kwanza kujua kuwa roho anakaa wapi?
Waefeso 3:16 kazi ya roho wake katika utu wa ndani.
1wakoritho 3:16 mmekuwa hekalu la Mungu na roho wa Mungu anakaa ndani yenu..
Kwa kadri ya maelezo ya aya hizo Biblia inaonyesha kuwa makazi halisi ya roho ni ndani ya miyoyo ya wanadamu hivyo kwa jumla hukaa ndani ya mtu.
Roho mtakatifu unena toka ndani ya mtu - utumia kinywa cha mtu
Matendo 1:16 alilo nena roho mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi…………
Marko 12:35-36 Daudi mwenyewe alisema kwa uweza wa roho mtakatifu.
Luka 12:12 kwakuwa roho mtakatifu atawafundisha ya pasayo kuyasema
Qur an 5:110…nilikupa roho takatifu ukaongea na watu maneno ya nafuu………..
Katika ushahidi huo wa aya za kibiblia tunaona jinsi roho wa Mungu anavyofanya kazi kwa kuwa ndani ya watu na hivyo kutumia vivywa vya watu hao katika kunena.
2Petro 1:20 Manabii walinena ya Mungu kwa kuongozwa na roho mtakatifu………..
Je roho alifanya majukumu hayo kupitia vinywa vya mitume mbalimbali?
-
Kuuhakikishia ulimwengu habari ya Haki
-
Dhambi na
-
Hukumu.
Kazi hizo roho anazitenda kwa kunena kupitia vinywa vya watu, maelezo ya kibiblia yanaweka wazi juu ya utekelezaji huo wa roho katika majukumu hayo..
Haki – Dhambi
Matendo 2:36-39
Katika andiko hili maarufu Biblia inaeleza juu ya kazi iliyotendwa na roho wa Mungu kupitia vinywa vya mitume wa Yesu pindi wakihubiri Injili na hivyo wale walosikia...
- Walihukumiwa kwa kuchomwa miyoyo yao – ( huko ndiko kuhakikisha kwa habari ya “dhambi).
- Roho aliwapa uongofu na kuhoji juu ya kile wanachopaswa kufanya – roho wa
Mungu aliwaongoza mitume kuwatangazia watu hao juu ya Haki “ubatizo” ili
wasamehewe dhambi zao na kupokea kipawa cha roho.
Mathayo 3:16- 18 kubali hivi sasa kwakuwa ndivyo ipasavyo kutimiza haki yote “ubatizo.
Hukumu
Kwa habari ya Hukumu maandiko ya Biblia yako wazi yakionyesha namna roho wa Mungu kupitia mitume wake alivyo fanya kazi ya kuhakikishia ulimwengu juu ya habari hiyo kama tunavyoweza kusoma:-
Rumi 8:1 Sasa basi hakuna Hukumu ya adhabu juu yao walio katika kristo
Yesu….
Qur an 43:61 na kwakweli yeye nabii Isa ndiye alama ya kiyama, ikifanyie shaka na
nifuateni hii ndiyo njia iliyonyooka.
-
Maelezo ya Qur an juu ya habari ya roho.
Pamoja na kile kinachoonekana ni kutaka kumpatia Muhammad fursa na madaraja ya juu katika utendaji wote na zaidi kumpa hadhi ya kibiblia, lakini bado busara zaidi inahitajika kwa kuyachunguza na kuyasoma maandiko ya kitabu cha Qur an chanyewe ili kitoe picha ya mwisho katika mada hii nyeti. Fatilia ushahidi huu ……..
Qur an 3:7 yeye ndiye aliyekutekemshia kitabu (hiki Qur an) ndani yake zimo aya
muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa kitabu
(hiki). Na ziko nyingine Mutashabihat (zinababaisha kama habari za
akhera, za peponi na motoni na mengine ambayo yamehusika na
“roho” …………..
Sidhani kama kuna kitu kingine kinachopasa kuchukua sehemu ya maandiko ya vitabu vinavyo aminiwa kwa kadri ya dini zetu. Andiko hilo la Qur an limeweka wazi vile ambavyo hata Qur an yenyewe inaonyesha
kutokuwa na mwanga thabiti kuhusiana na mambo ya roho, bilashaka hili ndilo linalopelekea hata mtume Muhammad mwenyewe kutoa tamko lake kuhusiana na habari hizo za roho.
Kwa hakika hapo ndipo tunapoweza kupima ukweli au udanganyifu wa fundisho la kudai kuwa utabiri wa Yohana ulikuwa ukimlenga Muhammad. hebu fatilia:-
Qur an 17:85 Na wanakuuliza habari za roho.sema roho ni jambo linlohusika na
Mola wangu (Mwenyezi Mungu) nanyi hamkupewa katika ilimu
(ujuzi) ila kidogo kabisa.( nayo no ilimu ya vitu visivyohusika na
roho).
Kibusara kauli ya mhusika haklisi inapaswa kuwa ndiyo ya mwisho,nami sasa ninaweza kufunga mjadala huu kwa kuishia katika kauli hiyo ya Muhammad inayo onesha tendo lake la kukataa kuhusika na habari za roho………
Roho halisi alikuja siku ya pentecoste na kuwashukia wanafunzi “Matendo 2:1”
Muhammad siye roho msaidizi aliyetabiriwa na Yesu – Mungu akubariki.